12.9 C
New York

Zelensky akosoa urafiki wa Trump, Putin

Published:

KYIV, Ukraine

RAIS wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amemwita Vladimir Putin kuwa ni muuaji, kauli aliyoitoa muda mfupi baada ya Donald Trumpo kusema kiongozi huyo wa Urusi ni Rafiki yake.

Katika mahojiano yake na kituo cha televisheni cha CNN, Zelensky amesema hamzuii Trump kumwita Rafiki, lakini Ukraine itaendelea kumtambua Putin kama adui na muuaji.

Hivi karibuni, Trump alikutana ana kwa ana na Putin, pamoja na Rais wa China, Xi Jinping, katika Mkutano uliofanyika katika nchi hiyo ya Asia.

Akizungumza baada ya Mkutano huo wa Alhamisi ya wiki hii, Trump alisema Putin ni rafiki yake wa miaka mingi.

Kauli hiyo imemchefua Zelensky, ambaye nchi yake inaendelea kuumizwa na mashambulizi makali yanayofanywa na jeshi la Urusi.

Moja ya mashambulizi hayo ni hili la jana Novemba 20, 2026, ambapo watu tisa nchini Ukraine walipoteza maisha baada ya Urusi kushambulia madaraja mjini Kyiv.

Related articles

Recent articles