16.4 C
New York

Marekani kuinyima misaada Israel

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

RAIS ⁠⁠Donald ⁠⁠Trump amesema alishamwambia Waziri wa Israel, Benjamin Netanyahu, kwamba Marekani itaacha kuwapa misaada ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Kwa miaka mingi, baadhi ya wanasiasa wa upinzani wa Democrat wamekuwa wakikosoa kitendo cha Israel kuiegemea Marekani kwa kupewa misaada.

“… Mimi na Netanyahu tulishakubaliana kwamba tutaipa Israel msaada wa Dola bilioni 4 na baada ya hapo tutaacha [kuipa misaada],” amesema Rais Trump.

Hata hivyo, wachambuzi wa siasa wamesema kauli ya Rais Trump haijaeleza ni misaada ipi ambayo Israel haitokuwa ikiipata kutoka kwa Marekani.

Kwa wengine, licha ya Rais Trump kutoka kauli hiyo, itachukua miaka mingi kuona Marekani ikisitisha moja kwa moja misaada yake ya kivita kwa Israel.

Related articles

Recent articles