16.4 C
New York

Nike yapigwa marufuku Libya

Published:

TRIPOLI, Libya

MAMLAKA za juu za kidini nchini Libya, Dar al-Ifta, imepiga marufuku waumini wa Kiislam kununua au kuuza mavazi yenye nembo ya kampuni ya Nike.

Kwa mujibu wa taasisi hiyo yenye makao makuu yake mjini Tripoli, Nike ni jina la mungu wa Kigiriki, ambaye mabawa yake yanawakilishwa na nembo ya kampuni hiyo ya Marekani.

Kile kilichoelezwa na Dar al-Ifta ni kwamba Muislam kuvaa nembo ya Nike ni sawa na kuunga mkono ushirikina.

Katia hatua nyingine, Kamati ya Dar al-Ifta imeishutumu Nike ikisema kampuni hiyo imekuwa ikiiunga mkono Israel.

Novemba, 2023, Baraza la Utafiti na Masomo ya Sharia nchini Libya liliwataka Waislam kutokushirikiana na kampuni zote zinazofanya kazi na Taifa hilo.

Dar al-Ifta ni taasi yenye nguvu, licha ya nchi ya Libya kugawanyika pande mbili, ambapo zipo mamlaka za Mashariki na zile za Magharibi, kila moja ikiamini ndiyo yenye haki ya kuongoza.

Related articles

Recent articles