16.4 C
New York

Yorke ataka Emery apewe United

Published:

MANCHESTER, Uingereza

LEJENDARI wa Manchester United, Dwight Yorke, amewashauri mabosi wa klabu hiyo kumpa ajira Unai Emery endapo wataamua kumfuta kazi Michael Carrick.

Carrick anapumulia mashine juu ya hatima yake Old Trafford baada ya Man United kukosa ushindi katika mechi tisa mfululizo [kabla ya kuivaa AS Roma].

Baada ya mechi yao dhidi ya Waitalia hao, Carrick na vijana wake watafunga safari kuifuata Aston Villa ya Emery katika mechi ya Ligi Kuu itakayochezwa wikiendi hii.

Yorke aliwahi kuitumikia Aston Villa kuanzia mwaka 1989 na 1998, kabla ya kuhamia Man United na kupata mafanikio makubwa.

Kwa upande wake, Yorke anaamini Man United ilipaswa kumpa kazi Emery badala ya Ruben Amorim aliyeajiriwa mwaka 2024.

“Nilisema muda mrefu. Nilisema miaka miwili na nusu iliyopita. Unai Emery alikuwa mtu sahihi kuliko Amorim,” amesema.

Related articles

Recent articles