16.4 C
New York

Mkongwe Chelsea akabidhiwa mikoba West Ham

Published:

LONDON, Uingereza

ALIYEWAHI kuwa kiungo mahiri wa Chelsea, Scott Parker, ataanza kibarua cha kuinoa West Ham United inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini England [Championship].

Taarifa zilizopo zinadai kuwa tayari mabosi wa West Ham wameshamalizana na Parker ili achukue mikoba ya Nuno Espirito Santo aliyefungashiwa virago.

Parker [46], aliwahi pia kuitumikia West Ham enzi zake akiwa mmoja ya viungo bora ndani ya Ligi Kuu ya England [EPL].

Ripoti zinaeleza kwamba Parker atatangazwa kuwa mkuu mpya wa benchi la ufundi kabla ya West Ham kuivaa Cardiff City.

West Ham iko kwenye hali mbaya msimu huu wa Championship kwani inashika nafasi ya nane kwenye msimamo ikiwa imekusanya pointi 22 pekee katika mechi 13.

Related articles

Recent articles