ISLAMABAD, Pakistan
WANANDOA Imaan Mazari na mumewe, Hadi Ali Chattha, ni wanasheria wa haki za binadamu, ambapo wamekuwa wakifanya kazi ya kutetea wanaharakati na hata waandishi wa habari wanaoingia matatani nchini Pakistan.
Sasa, wawili hao wamehukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani kila mmoja kwa mashitaka ya kujihusisha na vitendo vya ugaidi. Wamehukumiwa na Mahakama ya kukabiliana na ugaidi nchini humo.
Imaan na Chattha walifunguliwa mashitaka ya kuchochea vurugu na kutishia usalama wa taifa mwaka 2024.
Katika tukio la mwaka 2024, wawili hao walitajwa kutengeneza njama za kuidhuru timu ya taifa ya mchezo ya kriketi ya Uingereza ilipotembelea Pakistan.
Lakini, kwa mtazamo wa wengi, jumbe zao za kukosoa mamlaka na jeshi ndizo zilizosababisha wabambikiwe kesi.


