20.9 C
New York

Sita wafariki ajali ya helikopta huko India

Published:

NEW DELHI, India

MAHUJAJI watano na rubani mmoja wamepoteza maisha baada ya helikopta waliyokuwamo kuanguka huko Kaskazini mwa India.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi, ajali hiyo imetokea katika jimbo la Uttarakhand. Ilianguka muda mfupi baada ya kuondoka mjini Badrinath.

Ikitajwa kupoteza mawasiliano, bado chanzo halisi cha ajali hiyo hakijawekwa wazi, ingawa mamlaka zimetangaza kuchukua hatua za uchunguzi.

Kwa upande mwingine, vyanzo vingine vimetaja mvua kubwa ndiyo iliyosababisha. Uttarakhand ni Jimbo linalopakana na China na Nepal.

Kabla ya ajali hiyo, tayari mamlaka za hali ya hewa zilishaonya juu ya mvua, upepo mkali na radi.

Related articles

Recent articles