LOS ANGELES, Marekani
PAPA Leo XIV amekuwa kiongozi wa kwanza wa Kanisa Katoliki duniani kupiga kura katika Uchaguzi wa Marekani.
Kiongozi huyo raia wa Marekani, ambaye hivi karibuni alikuwa na uhusiano mbaya na Rais Donald Trump, alipiga kura yake kwa njia ya baruapepe mjini Illinois.
Ofisi yake imeeleza kuwa Papa ni muumini mkubwa wa haki na ushiriki wa wananchi katika mchakato huo wa kidemokrasia.
Ifahamike kuwa Papa Leo XIV ni raia wa kwanza wa Marekani kushika wadhifa wa kuliongoza Kanisa Katoliki baada ya kuchaguliwa Mei, 2025.
Hata hivyo, kwa nyakati mbalimbali, amekuwa akipaza sauti kukosoa utawala wa Rais Trump, ikiwamo hatua ya kuishambulia Iran.
Kura za awali zimeshaanza kupigwa lakini Uchaguzi rasmi unatarajiwa kufanyika Novemba 3, 2026.


