20.9 C
New York

Waziri aweka ngumu, agoma kujiuzulu

Published:

MADRID, Hispania

WAZIRI wa Uchukuzi wa Hispania, Oscar Puente, ameweka wazi msimamo wake wa kutokujiuzulu baada ya nchi hiyo kutikiswa na ajali mbaya ya treni mbili zilizogongana.

Katika ajali hiyo ya hivi karibuni, watu 69 walipoteza maisha, ikitajwa kuwa ni moja ya matukio mabaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Madrid, Oscar ameeleza kuwa bado kuna maswali mengi yanayohitaji majibu juu ya chanzo cha ajali hiyo.

“Jukumu langu kwa sasa si kuzungumzia hatima ya nafasi yangu, ni kuangalia namna ya kushughulikia tatizo,” amesema Waziri huyo.

Kauli yake hiyo inakuja wakati tayari kukiwapo kwa shinikizo kutoka kwa wakosoaji wake wanaomtaka kukaa pembeni.

Jumatano ya wiki hii, wananchi kadhaa waliandamana na kuizingira Ofisi yake wakiwa na ujumbe huo wa kushinikiza ajiuzulu.

Related articles

Recent articles