20.9 C
New York

Shearer aipa mtihani Liverpool

Published:

LONDON, Uingereza

LEJENDARI wa Newcastle United, Alan Shearer, anaamini Liverpool itahesabika kama timu yenye ubavu wa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England msimu huu endapo itaifunga Arsenal wikiendi hii.

Timu hizo zitakwaana Jumapili na Liverpool itashuka dimbani ikiwa na mwendo wa kushinda mechi tano mfululizo tangu ilipofungwa mabao 3-0 na Manchester City.

“Nafikiri nafasi nzuri kwa Liverpool kujiweka kwenye mazingira mazuri zaidi ni kwa kupata matokeo mazuri wikiendi hii,” amesema.

Wakati Man City ikiwa imekaa kileleni mwa msimamo wa Ligi ikiwa na pointi 21, Arsenal wako nafasi ya pili wakiwa na idadi hiyo ya pointi, tofauti ikiwa ni wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Kwa upande wao, Liverpool wako nafasi ya nne wakiwa na pointi 15, wakizidiwa moja tu na Brighton iliyoko juu yao.

Related articles

Recent articles