MANCHESTER, Uingereza
KLABU ya Manchester United inaiwania saini ya beki wa Fulham, Calvin Bassey, ukiwa ni mkakati wa kuimarisha safu yake ya ulinzi.
Bassey anayecheza maeneo mengi kwenye ulinzi, amekuwa pia akihusishwa na vigogo wa Ligi Kuu ya Italia [Serie A], Inter Milan.
Mkataba wake na Fulham ya jijini London utafikia ukomo mwishoni mwa msimu huu lakini klabu hiyo inataka kumshawishi aongeze mwingine wa mwaka mmoja.
Hata hivyo, mabosi wa Fulham hawaoni kama itakuwa rahisi kumbakiza nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 kutokana na nguvu ya pesa ya Man United na Inter.


