LONDON, Uingereza
TANGU ilipoanzishwa mwaka 1956, Ballon d’Or imekuwa ni tuzo yenye heshima kubwa katika ulimwengu wa soka na kwa miaka minne ya hivi karibuni, hakuna mchezaji wa taifa moja aliyebeba mara mbili.
Iko hivi; alichukua Lionel Messi wa Argentina mwaka 2023, akafuatiwa na Rodri wa Hispania [2024], Ousmane Dembele wa Ufaransa [2025], kisha Harry Kane wa England [2026].
Kwa hesabu rahisi, Argentina na Ufaransa ndizo nchi zinazoongoza kwa kutwaa Ballon d’Or [8], ikifuatiwa na Ureno, Ujerumani na Uholanzi, ambazo kila moja imeibeba mara saba.
England inafuata ikiwa na tano, kama ilivyo kwa Italia, huku Hispania, licha ya ukubwa wake kwenye soka, ikiwa na Ballon d’Or nne pekee.
Waingereza waliowahi kutwaa Ballon d’Or


