21.2 C
New York

Chris Brown ahukumiwa miezi nane

Published:

LOS ANGELES, Marekani

STAA wa muziki wa R&B, Chris Brown, amehukumiwa kifungo cha nje cha miezi nane nchini Uingereza.

Kilichomponza mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 37 ni kuhusika kwake katika shambulizi dhidi ya prodyuza wa muziki.

Taarifa zinaeleza kuwa Brown alihusika kumshambulia prodyuza Abraham Diaw katika tukio lililotokea katika ukumbi wa usiku jijini London mwaka 2023.

Baada ya kumkuta na hatia leo Oktoba 26, 2026, Mahakama imemuhukumu kifungo cha nje lakini huenda akafungwa gerezani endapo atakiuka masharti.

Aidha, mwalimu wake wa sauti, Omololu Akinlolu, naye ametajwa kuhusika katika tukio hilo, kwa mujibu wa waendesha mashitaka wa London.

Hivyo, Akinlolu mwenye umri wa miaka 40, naye amekumbana na hukumu ya miezi minne, huku kila mmoja akitakiwa kulipa faini ya Pauni 1,500.

Related articles

Recent articles