12.8 C
New York

John Cena: Hakuna wa kumzidi Pele

Published:

LOS ANGELES, Marekani

MKONGWE wa mchezo wa mieleka, John Cena, bado anaamini lejendari wa Brazil, Pele, ndiye mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea katika ulimwengu wa soka.

Pele aliyetwaa mataji matatu ya Kombe la Dunia akiwa na kikosi cha Brazil, alifariki mwaka 2022 akiwa na umri wa miaka 82.

Cena mwenye umri wa miaka 56, ametoa mtazamo wake huo wakati wa mahojiano na kituo cha televisheni cha talkSPORT. “Namchagua Pele,” amesema.

Hoja yake hiyo inakuja wakati ulimwengu wa soka ukiwa umegawanyika juu ya nani anapaswa heshima ya kuitwa mwanasoka bora wa muda wote.

Wakati wakongwe Pele na Diego Maradona wakizungumzwa, pia mjadala huo umewaingiza pia Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wanaotamba kwa sasa.

Related articles

Recent articles