13.1 C
New York

Messi hajapoa, atupia mbili Marekani

Published:

LONDON, Uingereza

LIONEL Messi amefunga mara mbili wakati timu yake ya Inter Miami ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya DC United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Marekani [MLS].

Messi [39], amepachika mabao hayo zikiwa ni siku nne tu tangu alipocheza mechi yake ya mwisho akiwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Argentina.

Katika mchezo huo dhidi ya DC United, mshambuliaji mwenzake wa zamani wa Barcelona, Luis Suarez, naye alifunga mabao mawili ya kipindi cha kwanza.

Kwa Messi, alifunga katika dakika ya 47 na 60 kukamilisha safari ya Inter Miami kuzisaka pointi tatu muhimu za mchezo huo.

Mshindi huyo mara nane wa tuzo ya Ballon d’Or, alikuwa nahodha wakati Argentina inatwaa ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2022.

Ameachana na majukumu ya kuitumikia Argentina akiwa amefunga mabao 126 katika mechi 208. Ndiye mchezaji aliyecheza mechi nyingi na mfungaji bora wa muda wote wa Taifa hilo.

Related articles

Recent articles