13.1 C
New York

Kipchoge avunja rekodi ya dunia

Published:

MELBOURNE, Australia

AKIWA na umri wa miaka 41, mwanariadha raia wa Kenya, Eliud Kipchoge, ameweka rekodi ya aina yake kwenye michuano ya Marathon ya Melbourne.

Staa huyo wa Kenya ameweka rekodi hiyo baada ya kutumia saa 2, dakika tisa na sekunde 10 kutwaa ubingwa wake wa 17 kwenye maisha yake ya riadha.

Huo umekuwa ubingwa wake wa kwanza tangu alipofanya maajabu katika mashindano ya Marathoni ya Berlin mwaka 2023.

“Naamini bado mwili wangu unaruhusu, bado naweza kushindana na kizazi kijacho,” amesema Kipchoge. “Mkongwe bado nashindana na nafurahi kushindana na vijana wa Gen Z.”

Nje ya riadha, Kipchoge amekuwa na Taasisi yake ya Eliud Kipchoge Foundation, ambayo imekuwa ikichagisha maendeleo ya elimu, mazingira na afya.

Related articles

Recent articles