BUENOS AIRES, Argentina
CHAMA cha Soka cha Argentina (AFA) kimempa ofa ya mkataba mpya kocha wa timu yake ya Taifa, Lionel Scaloni.
Scaloni [48], amekuwa kwenye benchi la timu hiyo tangu alipochukua mikoba ya Jorge Sampaoli mwaka 2018.
Kwa miaka nane aliyofanya kazi, ameiongoza Argentina kutwaa mataji makubwa manne, yakiwamo Kombe la Dunia na Copa America.
Julai, 2026, kocha huyo alikaribia kuipa taji la pili mfululizo la Kombe la Dunia lakini alipoteza rekodi hiyo walipofungwa bao 1-0 na Hispaia katika mechi ya fainali.
Alichokieleza mwandishi wa habari maarufu wa Argentina, Gaston Edul, ni kwamba AFA imempa ofa ya mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kukinoa kikosi hicho.
Endapo atasaini, ataiongoza timu hiyo kwenye fainali zijazo za Copa America za mwaka 2028, ambazo Argentina imetwaa ubingwa mara zote mbili mfululizo zilizopita.


