CATALUNYA, Hispania
KLABU ya Barcelona haijachana na mpango wake wa kumsajili mpachikaji mabao hatari wa Manchester City na timu ya Taifa ya Norway, Erling Haaland.
Barcelona, kama ilivyo Real Madrid, imejaribu mara kadhaa kumsajili Haaland lakini kipengele ni mkataba wake na Man City, ambao utafikia ukomo mwaka 2034.
Taarifa zinaeleza kuwa klabu hiyo ya Catalunya imepanga kumfuata Haaland kupitia usajili wa dirisha kubwa la kiangazi, 2027.
Aidha, ripoti zinadai kwamba kocha wa Barcelona, Hansi Flick, ni shabiki mkubwa wa Haaland na anatamani kuona akiingia katika kikosi chake.
Haaland mwenye umri wa miaka 26, ameshafunga mabao 168 katika mechi 2014 alizocheza akiwa na Man City. Kwa msimu huu, ameshaingia kambani mara sita.


