LONDON, Uingereza
WINGA wa Arsenal, Noni Madueke, anawindwa na klabu za Juventus na Atletico Madrid kuelekea dirisha dogo la usajili hapo Januari, 2027.
Madueke aliyesajiliwa na Arsenal mwaka 2025 akitokea Chelsea, amejikuta hana uhakika wa kuingia kikosi cha kwanza cha kocha Mikel Arteta na huenda akavutiwa kuondoka.
Msimu huu, mshambuliaji huyo amecheza dakika 23 pekee za Ligi Kuu ya England [EPL] na 22 ni zile za mchezo wa kwanza dhidi ya Coventry City.
Kwa sasa, nyota huyo raia wa England amebakiza miaka minne katika mkataba wake na Washika Bunduki hao wa Kaskazini mwa London.
Kile kilichoelezwa na mtandao wa CaughtOffside ni kwamba Madueke aliyewahi kucheza PSV Eindhoven amepokea ofa za klabu zingine za England.


