MADRID, Hispania
WASHIKA Bunduki wa London, Arsenal, wanamtolea macho mshambuliaji wa Real Madrid, Endrick, wakipanga kumfuata wakati wa usajili wa dirisha dogo la Januari, 2026.
Endrick [20], amejikuta akiwa hana uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza cha Madrid chini ya kocha raia wa Ureno, Jose Mourinho ‘Special One’.
Msimu uliopita, 2025-26, nyota huyo wa kimataifa wa Brazil alicheza kwa mkopo Lyon ya Ufaransa, ambako alionesha kiwango kizuri.
Wakati wa usajili wa kiangazi, 2026, Arsenal ilionesha nia ya kumsajili, ingawa ilikabiliwa na ushindani kutoka kwa klabu zingine kubwa za ndani na nje ya England.
Klabu za England zilizoonesha nia ya kumsajili ni Liverpool, Manchester City, Manchester United, Tottenham Hotspur, Aston Villa na Fulham.


