18.6 C
New York

Osimhen kuzikosa Madagascar, Guinea-Bissau

Published:

LAGOS, Nigeria

TIMU ya soka ya Taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’ itamkosa straika wake tishio, Victor Osimhen, katika mechi mbili zijazo za kufuzu fainali za AFCON 2027 kutokana na majeraha.

Eagles itakuwa nyumbani Alhamisi ya wiki ijayo kuivaa Madagascar, kabla ya kusafiri kuifuata Guinea-Bissau siku nne baadaye.

Osimhen alipata majeraha ya nyama za paja akiwa na klabu yake ya Galatasaray katika mchezo walioifunga Istanbul Başakşehir mabao 3-2.

Tangu siku hiyo, Septemba 4, 2026, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amekuwa nje ya uwanja akiuguza majeraha hayo.

Awali, kocha wa Eagles, Éric Chelle, alimwita kikosini, kabla ya kugundua kuwa ni mapema kumtumia katika mechi hizo.

Related articles

Recent articles