18.6 C
New York

Kinda United agombewa Ulaya

Published:

MANCHESTER, Uingereza

MSHAMBULIAJI chipukizi wa Manchester United, JJ Gabriel, ameingia kwenye rada za klabu kubwa nne barani Ulaya, ikiwamo Barcelona.

Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Sky Sports, Gabriel na wawakilishi wake tayari wako nchini Hispania kufuatilia dili la kujiunga na Wacatalunya hao.

Hata hivyo, ripoti zingine zinaeleza kuwa ‘dogo’ huyo mwenye umri wa miaka 15 ameingia pia kwenye mitego ya wapinzani wakubwa wa Barcelona, Real Madrid.

Kwa upande wake, PSG na Bayern Munich nazo zimetawa kuitaka saini ya mchezaji huyo anayekuja vizuri.

Hivi karibuni, ilielezwa kuwa wawakilishi wa Gabriel wameitaka Man United kumfungulia mlango wa kutoka kinda huyo.

Related articles

Recent articles