18.6 C
New York

Tottenham majanga tupu

Published:

LONDON, Uingereza

BAADA ya kufungwa mabao 3-2 na Aston Villa, Tottenham imefikisha mechi tano za msimu huu wa Ligi Kuu ya England bila kupata ushindi.

Kwa upande mwingine, kichapo hicho ni cha 50 katika mechi 141 za timu hiyo kwenye historia ya Ligi Kuu.

Tottenham wanapitia majanga hayo licha ya kwamba walitumia zaidi ya Pauni milioni 300 kusajili wachezaji wapya wakati wa usajili wa kiangazi uliofungwa hivi karibuni.

Mfululizo wa matokeo mabaya unaongeza presha zaidi kwa kocha wake raia wa Italia, Roberto De Zerbi, na sasa zipo tetesi kuwa huenda akapoteza kibarua.

Mchezo wa jana dhidi ya Villa ulipomalizika, kocha huyo alionja joto ya jiwe baada ya mashabiki wa Tottenham kuanza kuizomea timu yao.

Licha ya kumiliki mpira kwa asilimia 63.8, Tottenham walijikuta wakitanguliwa kwa mabao 3-0, kabla ya kusawazisha mawili kupitia kwa Conor Gallagher na Jan Paul van Hecke.

Related articles

Recent articles