18.6 C
New York

Gyokeres kutimkia Serie A?

Published:

LONDON, Uingereza

MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Viktor Gyokeres, anahusishwa na klabu nne za Ulaya, zikiwamo za Ligi Kuu ya Italia [Serie A].

Katika msimu wake wa kwanza Emirates, 2025-26, nyota huyo raia wa Sweden aliifungia Arsenal mabao 21 katika mechi 55 za mashindano mbalimbali.

Hata hivyo, bado nyota huyo hajaonekana kuwa chaguo la kwanza mbele ya nyota wa kimataifa wa Ujerumani, Kai Havertz.

Kwa mujibu wa vyanzo vya Habari barani Ulaya, AC Milan na Juventus ziko mstari wa mbele, kila moja ikimtazama kwa jicho la tamaa mshambuliaji huyo.

Wakati huo huo, inaelezwa kuwa zipo pia ofa kutoka kwa klabu tajiri za Ligi Kuu ya Saudi Arabia, Al Ittihad na Al Ahli.

Related articles

Recent articles