23.5 C
New York

Usajili wa bei mbaya unavyokosa matokeo Tottenham

Published:

LONDON, Uingereza

TOTTENHAM imepoteza mechi zote mbili ilizocheza msimu huu wa Ligi Kuu ya England. Ilifungua pazia kwa kufungwa mabao 3-0 na Brighton, kabla ya kichapo kingine cha 2-0 kutoka kwa Newcastle United.

Katika mchezo huo wa mwisho dhidi ya Newcastle, mashabiki wa Tottenham walionekana wakiondoka uwanjani kabla ya mchezo kumalizika, ikithibitisha kuwa hawakuvutiwa na kiwango cha timu yao.

Timu ambayo imetumia kitita cha zaidi ya Pauni milioni 300 katika dirisha kubwa la usajili wa kiangazi mwaka huu, ikiwanasa viungo Mateus Fernandes kutoka West Ham na Sandro Tonali aliyekuwa Newcastle.

Kwa pamoja, wawili hao wameigharimu Tottenham kiasi cha Pauni milioni 185, achilia mbali beki Jan Paul van Hecke kutoka Brighton (Pauni milioni 52) na winga aliyekuwa Manchester City, Savinho (Pauni milioni 75).

Pia, Tottenham imewanasa mabeki Marcos Senesi na Andy Robertson, pamoja na kipa Martin Dubravka, ambao hata hivyo walisajiliwa wakiwa wachezaji huru baada ya kumaliza mikataba katika timu walizotoka.

Wakati huo huo, wanaye Omar Marmoush waliyemchukua kwa mkopo kutoka Newcastle, ambaye kama atawika, basi watamsajili moja kwa moja kwa ada ya Pauni milioni 60 hapo mwakani.

Related articles

Recent articles