MADRID, Hispania
KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho, amesema mshambuliaji wake raia wa Ufaransa, Kylian Mbappe, anastahili tuzo ya mwaka huu ya Ballon d’Or.
Akizungumza kuelekea mechi yao na Malaga, Mourinho alimtaja Mbappe akisema ni mmoja ya wachezaji bora duniani alionao kikosini.
Mbappe amekuwa na mchango mkubwa wa mabao kwenye safu ya ushambuliaji ya Madrid tangu aliposajiliwa akitokea PSG ya Ufaransa.
“Kwa upande wangu, licha ya kuwa na wachezaji bora wengi, yupo mmoja aliyefanya makubwa zaidi kipindi hiki cha kiangazi,” amesema Mourinho akimzungumzia Mbappe.
Mourinho amerejea Santiago Bernabeu majira haya ya kiangazi lakini changamoto aliyonayo ni kurejesha taji la La Liga lililoko kwa majirani zao, Barcelona.


