22.6 C
New York

Desailly hamkubali hata kidogo kipa Chelsea

Published:

LONDON, Uingereza

LEJENDARI wa Chelsea, Marcel Desailly, amesema kama kuna mchezaji asiyetakiwa kuingia tena kwenye kikosi cha timu hiyo, basi ni kipa Robert Sanchez.

Kauli ya mkongwe huyo wa soka la Ufaransa inakuja wakati huu Chelsea wakiripotiwa kuwa kwenye hatua za mwisho za kumsajili kipa wa Aston Villa, Emiliano Martinez.

Sanchez alisajiliwa miaka mitatu iliyopita akitokea Brighton, ambapo usajili wake huo uliigharimu Chelsea kitita cha Pauni milioni 25.

Kipa huyo alionesha kiwango kisichovutia katika mechi yao ya kwanza msimu huu wa Ligi Kuu ya England, ambapo alichangia Fulham kupata mabao mawili, licha ya Chelsea kushinda 3-2.

“Naamini wanasubiri aimarike zaidi. Hata hivyo, inaumiza kuona kipa wa hadhi ya Ligi Kuu anashindwa kujiamini kana kwamba anacheza timu za vijan,” amesema Desailly.

Related articles

Recent articles