22.6 C
New York

Man United njia nyeupe kwa Adarabioyo

Published:

MANCHESTER, Uingereza

KLABU ya Manchester United imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kuinasa saini ya beki wa Chelsea, Tosin Adarabioyo.

Katika dirisha kubwa hili la usajili wa kiangazi, Man United imeelekeza nguvu kubwa katika eneo la kiungo kwa kuwanasas Youri Tielemans, Andrey Santos na Carlos Baleba.

Hata hivyo, zikiwa zimebaki siku chache kabla ya usajili kufungwa Septemba 1, 2026, imehamishia mipango kwenye safu ya ulinzi.

Kwa mujibu wa mwandishi maarufu wa habari za usajili wa Uingereza, Ben Jacobs, kwa sasa anatafutwa Adarabioyo anayecheza nafasi ya beki wa kati pale Chelsea.

Nyota huyo hakuwa sehemu ya kikosi cha Blues kilichopata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Fulham mwanzoni mwa wiki hii.

Hii si mara ya kwanza kwa Man United kuhusishwa na Adarabioyo kwani ilijaribu kumsajili mwaka 2024 lakini aliamua kutua Chelsea akitokea Fulham.

Chelsea, kwa upande wao, wameshaimarisha ‘ukuta’ wao kwa kuinasa saini ya beki wa kati kutoka Crystal Palace, Maxence Lacroix, usajili huo ukigharimu kiasi cha Pauni milioni 52.

Related articles

Recent articles