30 C
New York

PSG yazoa bil. 15/- kuifunga Villa

Published:

LONDON, Uingereza

KWA mujibu wa Gazeti la Daily Mirror, PSG ya kocha Luis Enrique imejiondokea na kitita cha Pauni milioni 4.3 (Zaidi ya Sh bil. 15 za Tanzania) kwa kutwaa taji la UEFA Super Cup usiku wa jana Agosti 12, 2026.

Mbali ya mkwanja huo, pia klabu hiyo ya jijini Paris, Ufaransa, imevuna kiasi cha Pauni 900,000 kama posho ya ubingwa wao huo.

PSG, mabingwa wa Ligi ya Mabingwa msimu uliopita, walikutana na Aston Villa iliyotwaa taji la Ligi ya Europa na kuifunga mabao 2-1.

Katika mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Red Bull, PSG ilipata mabao yake kupitia kwa Khvicha Kvaratskhelia na Desire Doue. Bao la Villa lilifungwa na Brian Madjo.

Kwa upande mwingine, matajiri hao wa Ligue 1 wanakuwa klabu ya tatu katika historia kutwaa mara mbili mfululizo ubingwa wa UEFA Super Cup baada ya Real Madrid na AC Milan kuwahi kufanya hivyo.

Hata hivyo, Villa ya kocha raia wa Hispania, Unai Emery, haijaondoka patupu kwani nayo imepata Pauni milioni 3.4, licha kupoteza mechi hiyo.

Related articles

Recent articles