LONDON, Uingereza
KWA miaka 43 sasa, rekodi ya dunia ya mbio ndefu za mita 800 kwa wanawake haijawahi kuvunjwa. Bado inashikiliwa na mwanariadha raia wa Jamhuri ya Czech, Jarmila Kratochvilova.
Kratochvilova aliweka rekodi hiyo mwaka 1983, alipomaliza mbio hizo akitumia dakika 53 na sekunde 28. Akiwa na umri wa miaka 32 tu wakati huo, alimzidi kwa sekunde saba Jolanta Januchta wa Poland aliyeshika nafasi ya pili.
Mwanariadha pekee walau aliyekaribia rekodi yake kwa miaka ya hivi karibuni ni Audrey Werro, ambaye hata hivyo alimaliza mbio za mita 800 akiwa ametumia saa 1, dakika 58, na sekunde 80.
Je, kwanini hakuna mwanariadha aliyeweza kumaliza ndani ya muda huo tangu Kratochvilova alipofanya hivyo wakati wa michuano ya dunia iliyofanyika mjini Munich, Ujerumani?
Licha ya kukanusha mara kadhaa, yaliibuka madai kuwa alitumia dawa za kuongeza nguvu, wakati huo Ujerumani ikiwa na sifa mbaya ya tabia za aina hiyo kwa wanamichezo wake.
Miaka miwili baada ya Kratochvilova kuandika historia hiyo, Mjerumani mwenzake, Marita Koch, naye aliandika rekodi yake katika mbio za mita 400.
Kama ilivyokuwa kwa Kratochvilova, ushindi wa Marita ulihusishwa na dawa lakini alipofanyiwa vipimo ilibainika kuwa hakuwa ametumia chochote.


