LOS ANGELES, Marekani
SUPASTAA wa muziki wa R&B, Chris Brown, amekutwa na hatia katika kesi ya kumshambulia mtu kwenye ukumbi wa starehe nyakati za usiku.
Brown anatajwa kumshambulia mtu kwa kumpiga na chupa ya kichwa katika tukio la mwaka 2023.
Polisi jijini London wamedai kuwa Brown na washikaji wake walifanya tukio hilo dhidi ya mwanaume.
Hata hivyo, nyota huyo wa muziki mwenye umri wa miaka 37 amekana shitaka hilo.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Brown anaweza kutupwa miaka mitatu gerezani wakati hukumu yake itakaposomwa Oktoba, 2026.


