TORONTO, Canada
HERVE Renard ametangaza kujiuzulu katika kibarua chake cha kuinoa timu ya soka ya Taifa ya Tunisia.
Mfaransa huyo ametema kibarua zikiwa ni siku 18 tu tangu alipoajiriwa kuchukua nafasi ya Sabri Lamouchi.
Lamouchi alifungashiwa virago baada ya timu hiyo kufungwa mabao 5-1 na Sweden katika mchezo wa kwanza msimu huu wa Kombe la Dunia (2026).
Renard (57), alipokea kijiti lakini hakuinusuru Tunisia kuishia hatua ya makundi baada ya kufungwa mechi mbili zilizofuata dhidi ya Japan na Uholanzi.
“Naitakia kila la kheri timu ya soka ya Taifa ya Tunisia. Ilikuwa ni heshima kubwa kuvaa jezi za Tunisia na kupata uzoefu huu,” amesema.


