MIAMI, Marekani
FAINALI za Kombe la Dunia za mwaka huu (2026) zimeandaliwa na nchi tatu; Marekani, Mexico na Canada.
Tangu michuano hiyo ianze mwaka 1930, nchi 19 zimeshapata fursa ya kuwa mwenyeji. Bara la Ulaya linaongoza kwa kuwa na mwenyeji mara 11.
Kwa mujibu wa historia, hii inakuwa mara ya tatu kwa Mexico kuwa mwenyeji na ndiyo nchi pekee kufanya hivyo tangu michuano hiyo ianze mwaka 1930.
Ukiacha hizi za mwaka huu, Taifa hilo la Amerika ya Kusini liliandaa fainali za mwaka 1970 na 1986, kwa mujibu wa tovuti ya Top End Sports.
Mataifa matano yanashika nafasi ya pili, kila moja likiwa mwenyeji mara mbili; Marekani (1994 na 2026), Ujerumani (1974 na 2006), Italia (1934 na 1990), Brazil (1950 na 2014), na Ufaransa (1938 na 1998).
Wakati huo huo, mataifa mengine 11 yameshawahi kuandaa fainali hizo mara moja kila moja.
Hapo unayataja Canada (2026), Qatar (2022), Urusi (2018), Afrika Kusini (2010), Japan na Korea ya Kusini (2002), Hispania (1982), na Argentina (1978).
Mengine ni England (1966), Chile (1962), Sweden (1958), Uswis (1954), na Uruguay (1930).
Fainali zijazo zitafanyika katika nchi tatu za Hispania, Ureno na Morocco. Wenyeji watatu kwa pamoja kama zilivyo za mwaka huu.
Miaka minne baadaye, 2034, michuano hiyo itaelekea Mashariki ya Kati kwa Saudi Arabia kuwa mwenyeji.


