32 C
New York

Scholes aitabiria majanga Arsenal msimu ujao

Published:

MANCHESTER, Uingereza

MKONGWE wa Manchester United, Paul Scholes, amesema haioni Arsenal ikitetea ubingwa, na badala yake itamaliza msimu ujao wa Ligi Kuu ya England (EPL) ikiwa nafasi ya nne kwenye msimamo.

Wakati huo huo, kiungo huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya England amedai kuwa bingwa wa msimu ujao ni Manchester United au Liverpool.

“Nafikiri Manchester United itakuwa na nafasi chini ya Michael (Carrick) endapo itafanya usajili mzuri. Liverpool natarajia wataamka.

“Man City itafanya vizuri, ingawa itakuwa na kocha mpya (Enzo Maresca). Watu wanatarajia Arsenal kutawala tena. Silioni hilo,” amesema Scholes.

Arsenal walitwaa ubingwa wa EPL wiki chache zilizopita, pia wakifika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya waliyopoteza kwa mikwaju ya penalti mbele ya PSG.

Related articles

Recent articles