BUDAPEST, Hungry
HIVI unafahamu kuwa hakuna timu ya soka ya taifa yenye wastani mzuri wa mabao ya kufunga kuliko Hungary katika historia ya fainali za Kombe la Dunia? Habari ndiyo hiyo.
Hungary, ambayo msimu huu haimo, ina jumla ya mabao 87 katika mechi 32 za Kombe la Dunia, sawa na wastani wa takribani mabao zaidi ya mawili katika kila dakika 90.
Hungary haijacheza Kombe la Dunia tangu mwaka 1986 lakini ilikuwa na kiwango bora zaidi cha upachikaji mabao iliposhiriki 1938, 1954 na 1982.
Katika michuano ya mwaka 1938 na 1954, timu hiyo ilifika hadi fainali lakini ilipoteza mbele ya Italia na Ujerumani (wakati huo ikiitwa Ujerumani Magharibi).
Hata hivyo, katika michuano ya mwaka 1983, Hungary ilimaliza ikiwa na mabao 15, ikiwamo kupata ushindi wa mabao 6-0 na 5-1.
Mwaka 1954, walimaliza wakiwa na mabao 27, ambapo katika baadhi ya mechi walishinda mabao 9-0 na 8-3.
Miaka nane baadaye, 1962, Hungary iliandika historia ya kuwa timu pekee kufunga mabao mengi katika mechi moja ya Kombe la Dunia ilipoifunga El Salvador mabao 10-1.


