28.1 C
New York

Galatasaray waitajia Chelsea dau la Osimhen

Published:

ISTANBUL, Uturuki

KLABU ya Galatasaray ya Ligi Kuu nchini Uturuki imeweka wazi dau la mshambuliaji wake wa kati anayetakiwa Chelsea, Victor Osimhen.

Galatasaray wametangaza kuhitaji euro milioni 150 ili kumwachia straika huyo wa kimataifa wa Nigeria.

Taarifa hizo zinakuja zikiwa ni siku chache zimepita tangu kocha wa timu ya Taifa ya Nigeria, Eric Chelle, alipofichua kuwa nyota huyo yuko kwenye mazungumzo na moja ya klabu za Ulaya.

Chelle alisema hajamuita Osimhen katika kikosi chake kitakachocheza mechi za kirafiki ili kumpa straika huyo nafasi ya kumalizia mazungumzo aliyonayo na klabu hiyo.

Hata hivyo, Osimhen amejitokeza na kuzungumzia kauli hiyo ya Chelle, akisema hakuna mazungumzo yanayoendelea.

Related articles

Recent articles