18.2 C
New York

Serengeti Boys v Senegal: Ni fainali ya aina gani AFCON?

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

TIMU ya soka ya Taifa ya U-17 ya Tanzania, Serengeti Boys, itashuka dimbani wikiendi hii, Juni 2, 2026, kumenyana na Senegal katika mchezo wa fainali ya AFCON ya vijana wa umri huo.

Kwa mujibu wa waratibu wa mashindano, Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), fainali itachezwa katika Uwanja wa Moulay El Hassan mjini Rabat.

Tayari Serengeti Boys na Senegal zimeshajihakishia tiketi ya kushiriki fainali zijazo za Kombe la Dunia za U-17 zitafanyika baadaye mwaka huu nchini Qatar.

Aidha, timu hizo zinakutana zikiwa zimetoka kushinda mechi ngumu za hatua ya nusu fainali zilizochezwa mjini Rabat, Morocco yanakofanyika mashindano hayo.

Serengeti Boys waliingia fainali yao ya kwanza katika historia ya michuano hiyo kwa kuifunga Misri kwa penalti 4-3 baada ya dakika 90 (hakuna 30 za nyongeza) kumalizika kwa timu hizo kutokufungana.

Kwa upande wao, Senegal waliwaondosha wenyeji wa michuano, Morocco, kwa staili hiyo hiyo ya penalti (7-6) baada ya sare ya bao 1-1 ndani ya uwanja.

Katika mchezo huo, Senegal walitangulia kwa bao la kipindi cha kwanza la Mouhamed Wagne, kabla ya Morocco kusawazisha dakika za jioni kupitia kwa Ismail El Aoud.

Related articles

Recent articles