MADRID, Hispania
NI rasmi Real Madrid imemrejesha Jose Mourinho kuwa kocha wao mpya na Mreno huyo amesaini mkataba wa miaka mitatu
Hata hivyo, ‘Special One’ mwenye umri wa miaka 63 atatangazwa rasmi baada ya Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo utakaofanyika Juni 7, 2026.
Mourinho, ambaye anaachana na Benfica aliyojiunga nayo Septemba, 2025, anarejea Santiago Bernabeu baada ya miaka 13 kupita.
Akiwa klabuni hapo kuanzia mwaka 2010 hadi 2013, aliiwezesha Madrid kutwaa mataji ya La Liga Copa del Rey na Spanish Super Cup.
Aidha, Benfica yake ilishika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Ureno msimu huu uliomalizika hivi karibuni.


