28.1 C
New York

Arteta: PSG hawasumbui, tumejipanga

Published:

LONDON, Uingereza

KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta, ana imani kubwa na kikosi chake, akisema wamejipanga kuikabili PSG na kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu wa 2025-26.

Baada ya ubingwa wa Ligi Kuu, Washika Bunduki wa London watakuwa dimbani Mei 30, 2026 kujaribu kutwaa kwa mara ya kwanza ubingwa wa Ligi ya Mabingwa.

Fainali hizo dhidi ya mabingwa watetezi, PSG, ni ya pili kwa Arsenal katika historia ya michuano hiyo. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2006, walipofungwa mabao 2-1 na Barcelona.

“Tuna nafasi nzuri ya kuandika historia mpya katika klabu yetu, na tunaamini kabisa, kwamba tunakwenda kufanikisha hilo,” amesema Arteta.

Arteta atakuwa kocha wa kwanza kuipa Arsenal ‘ndoo’ hiyo, kama alivyomaliza mkosi wa miaka 22 wa kulikosa taji la Ligi Kuu.

Related articles

Recent articles