12.9 C
New York

Casillas hataki hata kumsikia huyo Mourinho

Published:

MADRID, Hispania

KIPA wa zamani wa Real Madrid, Iker Casillas, ameibuka na majina ya makocha 10, ambao amesema wanastahili kuajiriwa na klabu hiyo kuliko kumpa kazi Jose Mourinho ‘Special One’.

Casillas ameyasema hayo wakati huu taarifa zikidai kuwa Madrid wako kwenye hatua za mwisho za kumtangaza. Mourinho kuwa kocha wao wa msimu ujao.

Wawili hao waliingia kwenye uhusiano mbaya wakati Mourinho akiinoa Madrid, hivyo kusababisha Casillas kuondoka katika klabu hiyo akiwa ameitumikia kwa miaka mingi.

Katika makocha aliosema wanafaa zaidi kuliko Mourinho, kipa huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Hispania amewataja Mikel Arteta, Unai Emery, Cesc Fabregas na Zinedine Zidane.

Kwa upande mwingine, Casillas amewazungumzia Vincent Kompany, Xabi Alonso, Iraola, Bordalas, Inigo Perez na Del Bosque.

Related articles

Recent articles