13.5 C
New York

Guardiola atatua wapi akiondoka Man City?

Published:

MANCHESTER, Uingereza

PEP Guardiola amekamilisha projekti aliyopewa wakati anaajiriwa na Manchester City mwaka 2016. Kuifanya klabu hiyo kuwa tishio barani Ulaya. Amefanikiwa.

Wakati huu akijiandaa kuondoka, anaiacha Man City ikiwa na jumla ya mataji 20 tangu alipoanza kazi. Sita ni ya Ligi Kuu. Matatu ya FA. Matano ya Kombe la Ligi. Moja ni la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Amefanikiwa.

Lakini je, ipi hatima ya Guardiola? Mhispania huyo atatimkia wapi baada ya kuachana na Man City?

Zipo taarifa zinazomuhusisha na klabu za Ligi Kuu ya Italia (Serie A) na Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1). Je, inawezekana kwa Mhispania huyo kuibukia huko?

Soka la Italia limekuwa nyumbani kwa makocha wengi wakubwa katika miaka ya hivi karibuni. Antonio Conte, Massimiliano Allegri na Jose Mourinho ni miongoni mwao.

Hata hivyo, kwa klabu kubwa za AC Milan, Juventus au Inter Milan, changamoto inaweza kuwa kwenye msuli wa kiuchumi wa kukabiliana na nahitaji ya Guardiola.

Kwa Ufaransa, PSG Ina uwezo wa kifedha wa kumpa kazi Guardiola lakini tayari wanaye Luis Enrique anayefanya vizuri klabuni hapo.

Katika hatua nyingine, Guardiola anahusishwa na klabu kubwa mbili alizowahi kufanya kazi. Barcelona ya La Liga na Bayern Munich ya Bundesliga.

Guardiola kurudi Barcelona zimekuwa ni taarifa za kila msimu unapokwisha. Ni klabu iliyoibua kipaji chake cha ufundishaji soka, pia akiipa mafanikio makubwa akiwa kocha wake.

Hata hivyo, kocha wa sasa raia wa Ujerumani, Hansi Flick, anafanya kazi nzuri. Ameipa taji la La Liga misimu yote miwili mfululizo aliyokaa kwenye benchi.

Kwa Bayern Munich ya Bundesliga, ambayo pia aliwahi kuinoa, uwezekano wa kurudi ni mdogo. Timu hiyo inafanya vizuri kwa sasa chini ya kocha Vincent Kompany.

Related articles

Recent articles