25.4 C
New York

Huyu hapa ndiye mchezaji mfupi zaidi NBA

Published:

LOS ANGELES, Marekani

WAKATI urefu ukionekana kuwa moja ya vigezo muhimu kwenye mchezo wa mpira wa kikapu, Muggsy Bogues anabaki kuwa mchezaji mfupi zaidi kuwahi kucheza na kuwika NBA (Ligi Kuu ya Kikapu ya Marekani).

Akiwa na urefu wa futi 5 na inchi 3 tu, Borgues alitamba NBA kwa miaka 14 tangu aliposajiliwa kwa mara ya kwanza na Washington Bullets (sasa ikiitwa Wizards) mwaka 1987.

Kwa miaka 14 hiyo, alipita katika klabu kubwa za Charlotte Hornets, Golden State Warriors na Toronto Raptors, ambapo licha ya kimo chake, alifunga pointi 24 na asisti 19 katika mechi tatu tofauti katika maisha yake ya NBA.

Nyota wengine waliowahi kucheza NBA kwa mafanikio wakiwa wafupi ni Earl Boykins (futi 5 na inchi 5), Spud Webb, Mel Hirsch na Greg Grant (futi 5 na inchi 6 kila mmoja).

Wengine kwenye ‘Top 10’ ni Keith Jennings, Red Klotz, Wat Misaka, Markquis Nowell na Monte Towe, kila mmoja akiwa na urefu wa futi 5 na inchi 7.

Kwa upande mwingine, Zach Edey wa Memphis Grizzlies na Victor Wembanyama anayecheza San Antonio Spurs ndiyo wachezaji warefu zaidi kwa sasa NBA, kila mmoja akiwa na urefu wa futi 7 na inchi 4.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img