25.4 C
New York

Man United ya Carrick msimu ujao balaa tupu

Published:

MANCHESTER, Uingereza

NI suala la muda tu kabla ya Manchester United kumtangaza Michael Carrick kuwa kocha wao wa msimu ujao (2026-27) baada ya kazi nzuri aliyoifanya tangu alipokalia kwa muda kiti cha Ruben Amorim.

Kubwa zaidi, Carrick ameirejesha Man United kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, hivyo kuibua matumaini mapya kwa timu hiyo.Man United ya Carrick msimu ujao balaa tupu

MANCHESTER, Uingereza

NI suala la muda tu kabla ya Manchester United kumtangaza Michael Carrick kuwa kocha wao wa msimu ujao (2026-27) baada ya kazi nzuri aliyoifanya tangu alipokalia kwa muda kiti cha Ruben Amorim.

Kubwa zaidi, Carrick ameirejesha Man United kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, hivyo kuibua matumaini mapya kwa timu hiyo.

MASTAA WATAKAOONDOKA KIANGAZI

Carrick amethibitisha kuwa Tyrell Malacia ataongozana na Casemiro kuondoka Man United mwishoni mwa msimu huu. Ni kama ilivyo kwa Jadon Sancho na Rasmus Hojlund anayecheza kwa mkopo Napoli.

Vilevile, ripoti zinaeleza kuwa Carrick Hana mpango wa kumrejesha kipa raia wa Cameroon, Andre Onana, na hata mshambuliaji anayecheza kwa mkopo Barcelona, Marcus Rashford. Nyota wengine wanaotazamiwa kutimka ni Joshua Zirkzee, Manuel Ugarte, Mason Mount na Altay Bayindir.

 HAYA HAPA MAJEMBE MAPYA

Wachezaji wote waliosajiliwa majira ya kiangazi, 2025, wameonesha viwango bora. Nyota hao ni Matheus Cunha, Bryan Mbeumo, Benjamin Sesko na Senne Lammens.

Hata hivyo, bado Man United italazimika kuingia sokoni majira ya kiangazi, 2026, kuongeza viungo wa kati wawili au watatu.

Miongoni mwa wanaohusishwa nao kwa sasa ni Carlos Baleba (Brighton), Ederson (Atalanta), Adam Wharton (Crystal Palace), Mateus Fernandes (West Ham) na Aurelien Tchouameni (Real Madrid).

Ukiweka kando usajili wa kiungo, Man United inataka winga wa kushoto wa kumsaidia beki Luke Shaw. Patrick Dorgu ni mzuri katika kushambulia lakini ameshindwa mara kadhaa majukumu ya ulinzi.

Katika hatua nyingine, huenda Carrick akaongeza kipa wa kusaidiana na Lammens, pia mshambuliaji wa kati wa kumpa changamoto Sesko.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img