LONDON, Uingereza
KOCHA wa muda wa Chelsea, Calum McFarlane, amesema hawana cha kuambulia msimu huu zaidi ya Kombe la FA, hivyo lazima wapambane kuifunga Manchester City wikiendi hii.
Timu hizo zitakutana Jumapili ya Mei 17, 2026, katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Wembley.
“Ni fainali ya FA, kwa hiyo tunataka kushinda. Ni michuano mikubwa, yenye heshima kubwa na klabu Ina historia nayo, ikiwa imetwaa ubingwa mara nane.
Chelsea imekuwa na mwenendo usioridhisha msimu huu wa Ligi Kuu ya England lakini wametoka kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Liverpool.
Kwa upande mwingine, McFarlane amegoma kuzungumzia tetesi za makocha wanaohusishwa kuiona Chelsea msimu ujao.
Licha ya kukiri kuwa Blues inahusishwa na Xabi Alonso, Cesc Fabregas na Xavi, Muingereza huyo amesema: “Siwajibiki kusema nani atakuwa kocha mpya.”


