21.4 C
New York

Osimhen atakiwa kuondoka Uturuki

Published:

ISTANBUL, Uturuki

MKONGWE wa Inter Milan, Obinna Nsofor, amemshauri Mnigeria mwenzake, Victor Osimhen, kuondoka Galatasaray, akisema ameshafanya makubwa Ligi Kuu ya Uturuki (Super Lig).

Osimhen ameshinda mara mbili mfululizo taji la Super Lig tangu alipojiunga na Galatasaray akitokea Napoli, na sasa anawindwa na klabu za Real Madrid, Bayern Munich, Chelsea na Manchester United.

“Victor Osimhen amefanya makubwa akiwa na Galatasaray. Kama anataka kuwa straika mkubwa zaidi duniani, anapaswa kujiunga na klabu yenye ushindani Ligi ya Mabingwa Ulaya,” amesema Nsofor.

Lejendari huyo aliyewahi pia kupita West Ham United, amesema licha ya ukubwa wa Galatasaray, bado klabu hiyo haiwezi kumpa Osimhen taji la Ligi ya Mabingwa.

“Galatasaray ni klabu kubwa, hakuna anayeweza kupinga hilo, lakini huwezi kuitaja unapozungumzia klabu zenye nafasi ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa,” amesema.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img