23.8 C
New York

Arsenal, Man City hakuna kulala ubingwa EPL

Published:

LONDON, Uingereza

BAADA ya Manchester City kuinyuka Manchester City mabao 3-0, sasa presha imerudi kwa Arsenal iliyoko kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England (EPL).

Kila timu imebakiza mechi mbili na ni pointi mbili tu zinazozitenganisha Arsenal na Man City katika nafasi ya kwanza na ya pili kwenye msimamo.

Arsenal watakuwa mabingwa wa EPL kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2003-04 ikiwa watashinda mechi mbili zilizobaki – dhidi ya Burnley na Crystal Palace.

Lakini pia, endapo watashinda mechi ya Jumatatu ijayo dhidi ya Burnely, kisha Man City ikashindwa kuifunga Bournemouth katika mchezo wa kesho yake, basi Mikel Arteta na vijana wake watatangaza ubingwa wa EPL msimu huu wa EPL.

Kinyume chake, ikiwa Arsenal na Man City, basi vita ya ubingwa itaamuliwa katika mechi za mwisho zitakazochezwa Mei 24, 2026, ambapo Pep Guardiola na vijana wake watakuwa Etihad kukabiliana na Aston Villa.

Related articles

Recent articles