9.5 C
New York

Enzo atamani kutimkia Real Madrid

Published:

LONDON, Uingereza

KIUNGO wa Chelsea, Enzo Fernandez, inaelezwa kuwa ni ndoto yake kubwa kujiunga na vigogo wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga), Real Madrid.

Taarifa za kuondoka kwake Stamford Bridge zimekuwa nyingi katika siku za hivi karibuni, akihusishwa pia na klabu za Serie A, ikiwamo Napoli.

Chelsea wanapitia wakati mgumu msimu huu, ambapo tayari wameshapoteza mechi nne mfululizo, wakishika nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu ya England (EPL).

Madrid, mabingwa mara 15 wa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, wanamtolea macho Muargentina huyo ili kuimarisha eneo lao la kiungo.

Wakati huu klabu za Ligi Kuu ya Saudi Arabia nazo zikihusishwa naye, Enzo mwenye umri wa miaka 25 ameonesha kuvutiwa zaidi na Madrid.

Hata hivyo, licha ya Madrid kuripotiwa kumpigia hesabu, taarifa zinadai kuwa bado hakuna ofa waliyowasilisha mezani kwa mabosi wa Blues.

Nyota huyo alisaini mkataba mrefu wa miaka nane aliposajiliwa na Blues mwaka 2023 na hivi karibuni aliongeza mwaka mmoja.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img