LONDON, Uingereza
LEICESTER City imeshuka kutoka Championship (Daraja la Kwanza England) hadi League One (Daraja la Pili). Hali ni tete kwao.
Hata hivyo, licha ya mwenendo mbaya wa timu hiyo, kiungo wake raia wa England, Harry Winks, analipwa Pauni 90,000 kwa wiki.
Kwa mshahara huo, Winks amewaacha mbali wachezaji wengi wenye majina makubwa wanaokipiga Ligi Kuu ya England (EPL).
NICO O’REILLY (MAN CITY)
Beki wa kushoto anayefanya vizuri EPL akiwa na kikosi cha Manchester City. O’Reilly ana umri wa miaka 21 tu lakini anatajwa katika orodha ya wanaoweza kuibeba tuzo ya Mchezaji Bora wa msimu huu.
Hata hivyo, O’Reilly si miongoni mwa wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa Man City. Anapokea Pauni 30,000 tu kwa wiki.
MARTIN ZUBIMENDI (ARSENAL)
Arsenal walimng’oa Real Sociedad kwa Pauni milioni 51 na sasa ni mchezaji tegemeo kwenye eneo la kiungo la kikosi cha kocha Mikel Arteta.
Hata hivyo, mshahara wa kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 27 ni Pauni 75,000 tu kwa wiki.
ADAM WHARTON (CRYSTAL PALACE)
Mmoja ya viungo bora EPL kwa sasa. Wharton alisajiliwa na Palace mwaka 2024 akitokea Blackburn Rovers.
Kwa kazi yake nzuri ndani ya uwanja, mabosi wa Palace wanamlipa kitita cha Pauni 35,000 kwa wiki.
JEREMY DOKU (MAN CITY)
Winga wa Man City. Alisajiliwa na klabu hiyo mwaka 2023 akitokea Ligue 1 alikokuwa akiitumikia Renens.
Akiwa na moja ya klabu tajiri Ulaya, kwa sasa nyota huyo raia wa Uholanzi anatajwa kulipwa Pauni 500,000 kwa wiki.


