5.5 C
New York

HaloPesa yawawezesha mahitaji ya Sikukuu wakazi wa Visiga

Published:

Na Iman Nathaniel, Gazetini

KUELEKEA sikukuu ya Eid El Fitr, Kampuni ya Halotel kupitia HaloPesa imetoa msaada wa mahitaji muhimu kwa familia zaidi ya 60 katika Kata ya Visiga (Visiga A na Visiga B) Wilaya ya Kibaha, Pwani.

Lengo la kufanya hivyo ni kusaidia familia zenye uhitaji kwa kuwapatia mahitaji ya msingi ya chakula, ikiwemo mchele, mafuta ya kupikia, sukari pamoja na bidhaa nyingine muhimu, ili kuwawezesha kusherehekea sikukuu ya Eid kwa furaha, amani na heshima.

Tukio hilo liliongozwa na Meneja Masoko wa HaloPesa, Aidat Lwiza, kwa kushirikiana na Meneja wa Halotel Mkoa wa Pwani, Rodrique Paul, pamoja na timu nzima ya kampuni hiyo, pamoja na viongozi wa Serikali za mitaa akiwamo Diwani wa eneo hilo, Mohamed Mpaki.

Akizungumza katika hafla hiyo, Aidat amesema “Mwisho wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni kipindi cha kuonesha upendo, huruma na mshikamano. HaloPesa inaamini kuwa mafanikio ya biashara yanaenda sambamba na ustawi wa jamii. Kupitia mpango huu, tunalenga kugusa maisha ya familia hizi na kuhakikisha wanasherehekea sikukuu kwa furaha na aman,” amesema.

Naye Kwa upande wake, Meneja wa Halotel Mkoa wa Pwani, amesema ushirikiano huo unaonesha dhamira ya dhati ya kampuni hiyo katika kuendelea kuwa karibu na jamii, kujenga mshikamano na kusaidia wale wenye uhitaji katika maeneo wanayohudumia.

Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo, Mpaki, aliipongeza HaloPesa kwa jitihada hizo na kusisitiza umuhimu wa sekta binafsi kushirikiana na jamii katika kuleta maendeleo jumuishi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img