6.4 C
New York

Petit: Arteta ataondoka Arsenal

Published:

LONDON, Uingereza

KIUNGO wa zamani wa Arsenal, Emmanuel Petit, amesema ni jambo lisiloepukika kwa Mikel Arteta kuondoka klabuni hapo.

Wakati huo huo, Mfaransa huyo amemshauri Arteta kutimkia Barcelona ya Ligi Kuu nchini Hispania (La Liga).

“Siku moja Mikel Arteta atainoa Barcelona. Tutaona hilo likitokea. Ana uhusiano mzuri nao,” amesema Petit.

Chini ya Arteta, Arsenal ya msimu huu inafukuzia mataji manne, ambayo ni Ligi ya Mabingwa, Ligi Kuu, FA na Kombe la Ligi (EFL Cup).

Hata hivyo, Mhispania huyo alikarahishwa na kiwango kibovu walichoonesha vijana wake katika mchezo uliopita wa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Wolves.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img